Habari

ACT Wazalendo wapishana na CHADEMA kuhusu uchaguzi jimbo la Kinondoni na Siha

Wakati zikiwa zimepita siku tatu tangu CHADEMA watangaze kuwa watashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Kinondoni na Siha leo Chama cha ACT-Wazalendo kimeendelea kushikiria msimamo wao wa kutoshiriki kwenye uchaguzi huo kwa kuwa sababu zilizowafanya wasusie uchaguzi mdogo uliopita, bado hazijafanyiwa kazi.

Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Bara, Msafiri Mtemelwa

Akizungumza na waandishi wa habari leo jumapili Januari 21, 2018. Naibu Katibu Mkuu waATC Wazalendo Bara, Msafiri Mtemelwa amesema changamoto walizolalamikia katika uchaguzi mdogo uliofanyika Januari 13 katika majimbo ya Songea Mjini, Longido na Singida Kaskazini bado hazijafanyiwa kazi.

Mtemelwa amesema bado chama hicho kitaendelea kushinikiza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufanya mageuzi katika mchakato wa uchaguzi.

Soma na hii – CHADEMA wakubali kushiriki uchaguzi, Wasimamisha wagombea Kinondoni na Siha

ACT Wazalendo walilalamikia kuwa kuna matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya vyama vya upinzani kwa lengo la kukisaidia chama tawala CCM.

Majimbo ya Siha na Kindondoni yalikuwa wazi baada ya waliokuwa wabunge wa majimbo hayo kuhamia CCM mwishoni mwa mwaka jana.
soma zaidi – ACT Wazalendo wasusia kushiriki uchaguzi mdogo wa majimbo matatu, waeleza sababu

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents