Fahamu

Facts: Mambo 12 ambayo wafuatiliaji wengi wa hip hop hawayajui

Bila shaka hip hop ni muziki ambao una mashabiki wengi zaidi duniani kutokana na kugusa maisha ya wengi.

Wafuatailiaji wa muziki huo  wamekuwa katika msisimko wa aina yake miaka nenda rudi, hata hivyo kuna baadhi ya vitu vya nyuma ya pazia ambayo hawavijui. Hapa nimekuwekea mambo 12 ambayo wafuatiliaji wengi wa hip hop hawayajui.

  1. Msanii Shaq amewahi kufikisha mauzo ya platinum katika album wakati Gang Starr hajawahi kufanya hivyo, Shaq alifanya hivyo kupitia albamu yake Shaq Diesel.

2. Usiku ambao Tupac alifariki Las Vegas, mchumba wake Kidada Jones alimuuliza kama anaweza kuvaa bulletproof lakini rapper huyo alimueleza kuwa  ina joto sana.

3. Inaelezwa kuwa rapper Eazy–Z hukuwahi kuandika mwenyewe mistari ya ngoma zake.

4. Dr. Dre ametengeneza fedha nyingi zaidi kwa kuuza headphones zake kuliko kwenye muziki.

5. Nas alikuwa rapper wa kwanza kutoka New York kusikika katika wimbo wa Dr. Dre.

6. Humchukua dakika 15 Kanye West kutengeneza beat.

7. Rapper Eminem alikuwa amevaa bullet proof studio wakati wakitengeneza ngoma ‘Moment of Clarity’ na Jay Z.

8. Jay-Z na Busta Rhymes walisoma shule ya sekondari pamoja na mara kwa mara walikuwa wakichanana katika mgahawa wa shule, pia DMX na Biggie walisoma pamoja.

9. J Cole alihudhuria Chuo Kikuu cha St. John ambapo alihitimu mwaka 2015 kwa kupata GPA ya 3.82.

10. Dr. Dre hukaa studio kwa saa 79 bila kulala/kuonekana.

11. Aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama anafikiri kuwa rapper Kendrick Lamar anamshinda Drake katika michano.

https://twitter.com/OnlyHipHopFacts/status/818977729223737344?ref_src=twsrc%5Etfw&ref_url=https%3A%2F%2Fwww.buzzfeed.com%2Fpedrofequiere%2Fyall-dont-even-know-the-ledge

12. Rapper Snoop Dog hajawahi kushinda tuzo ya Grammy.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents