Burudani
Afrika hakuna tena Big Three – Rema
Ni Headlines za Hitmaker wa (Calm Down) Rema akisema sasa hivi Muziki wa Afrika hauna tena ile (Big Three) “Davido, Burna Boy na Wizkid” bali kuna Big Four akiongeza jina lake katika List hiyo ya wasanii wakubwa.
“Hakuna Big 3 sasa kuna Big 4” ameandika Rema.
Story nyingine kuhusu Rema amefunguka kwamba amebadilisha Muziki wa Afrika (Afrobeats) kuanzia Sound, Shows na Brand.
Pia anajua watu Wengi wanaiga style yake na anafurahishwa na jambo hilo ila anajua hawawezi kumpa utukufu na maua yake mapema.
Imeandikwa na Mbanga B.