Michezo

Juma Mgunda ndiye Kocha bora kwenye Ligi ya Tanzania – Ahmed Ally

Juma Mgunda ndiye Kocha bora Tanzania hivi sasa.

Kocha Mgunda alianza msimu akiwa na timu ya Simba Queens na ameiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa akiwa hajapoteza mechi hata moja.

Baada ya kuipa Ubingwa Simba Queens, sasa yupo Simba Senior team na amefanya mabadiliko makubwa kwenye timu.

Ameweza kunyanyua viwango vya wachezaji na ataiwezesha Simba kumaliza nafasi ya mbili za juu.

Ni Kocha mwenye uwezo wa kuzalisha kutengeneza na kuendeleza kipaji cha mchezaji.

Kufundisha  Wanaume na Wanawake ndani ya msimu mmoja na wote wakapata mafanikio sio jambo jepesi na sio kila Kocha anaweza ni Juma Mgunda pekee.

Inaweza kuja hoja ya Ubingwa lakini haina mashiko, kuna Mbwana Makata alikuwa bora kwa sababu ya kuinusuru Kagera Sugar kushuka Daraja , Mecky Mexime aliwahi Kuwa Kocha Bora kwa kuzalisha kuendeleza vipaji na kutengeneza Mtibwa Sugar kuwa timu tishio kama anavyofanya Mgunda hivi sasa.

Sababu ya mwisho kwanini Juma Mgunda ndio Kocha bora ni nidhamu na heshima aliyonayo.

Kocha Mgunda hajawahi kutukana Mwamuzi, hajawahi kupigana na wala hajawahi kuingia uwanjani kufanya vurugu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents