Michezo

Yaliyomkuta Benchikha Simba SC

CONFIRMED: KLABU ya Simba imetangaza kufikia makubaliano ya pande mbili kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Mualgeria, Abdelhak Benchikha ikiwa ni siku moja tangu atwae Kombe la Muungano lililohitimishwa jana visiwani Zanzibar huku Juma Mgunda akipewa timu hiyo.

Klabu hiyo imeachana na Benchikha kwa kile ARENA inachofahamu kwamba ni kutokana na matatizo yake ya kifamilia kwao Algeria na hivyo kudumu kwa siku 156 tangu alipotambulishwa Novemba 24, mwaka jana akichukua nafasi ya Robertinho Oliveira ‘Oliveira.

Benchikha anatarajiwa kuondoka na benchi lake la ufundi lote na Simba inatarajiwa kuwa chini ya Juma Mgunda na Suleiman Matola wakati ikimsaka kocha mpya.
Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents