Michezo

Hakuna kama Mgunda kwa sasa – Ahmed Ally

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amesema kuwa kaimu Kocha Mkuu wa Simba Juma Mgunda amefanyia kazi mapungufu waliokuwa nayo timu hiyo ikiwa ni pamoja na tatizo la kuruhusu mabao kila mechi.

Ahmed amesema hayo mara baada ya Simba kuichapa Azam FC mabao 3-0 mchezo wao wa Ligi uliopigwa jana katika Dimba la Mkapa na kuongeza kuwa, Simba sasa imeimarika na kurejesha makali yake.

“Alichoanza nacho Kocha Mgunda ni kurekebisha safu ya Ulinzi na kupunguza idadi ya mabao. Tulikuwa tunafungwa mabao karibu kila mechi tangu msimu umeanza Mgunda aliamua kufanyia kazi hilo.

“Mipango yake iligoma Namungo tukatoka 2-2 lakini Tabora alikuwa 2-0 na leo hii Azam anakufa 3-0 maana yake mabadiliko ya Mgunda yamefanya kazi asilimia 100 na sasa Simba imesimama¬† kwenye mstari wake” amesema Ahmed Ally.

Katika msimamo wa Ligi Yanga wanaongoza wakiwa na alama 68 katika michezo 25 Azam nafasi ya pili alama 57 na michezo 26 huku Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 56.

Mchezo unaofuata wa Ligi kuu Tanzania Bara kwa timu ya Simba SC ni dhidi ya Kagera Sugar FC unaotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili ya Mei 12, 2024.

 

Video kamili bonyeza Link hapa chini:

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents