Habari

Akerwa damu kuhifadhiwa kwenye jokofu la matumizi ya nyumbani hospitalini Tanga

Mkurugenzi wa huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume amekerwa na kitendo cha uhifadhi damu kwenye jokofu la matumizi nyumbani.

Hayo yamebainika katika Hospitali ya halmashauri ya mji Korogwe Magunga wakati wa ziara mkoani humo.

Dkt. Mfaume ameonesha kukerwa na kutoridhishwa na kitendo hicho na kuelekeza kufanyika utaratibu wa haraka wa upatikanaji ya jokofu maalumu kwa kuhifadia damu.

“Hili jokofu ambalo mnatunzia damu ni kama tulilolikuta kule na hii tumeletewa na mdau lakini ni jokofu ambalo aliyetengeneza pale chini ‘fresh vegetables’ yaani mbogamboga kama mchicha tumetoka kule Shinyanga Mwalugulu tumewasema tukajua huku mmejifunza mtahangaika na sisi hatutaki kuona haya yanayofanyika huku tuyaone sehemu nyingine lakini mnaonekana Korogwe TC mnawataalamu wa kununua domestic fliji na kuhifadhi maabara tumeenda tumekuta majokofu sita jumla Domestic” amesema Dkt. Mfaume.

Ikumbukwe Aprili 2024 wakati wa ziara ya usimamizi shirikishi katika Mkoa wa Shinyanga timu ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilibaini ukiukwaji ma manunuzi ya majokofu ya kuhifadhia damu katika kituo cha afya Mwalugulu kilichopo halmashauri ya Msalala.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents