Michezo

Nini kinafuata baada ya kuondoka Benchikha?? – Edo Kumwembe

“Nini kinafuata? Kuondoka kwake (Benchikha) kunaipa Simba nafasi ya kuanza upya. Naambiwa Simba wamepania kuachana na kundi kubwa la wachezaji ambao wanaamini hawana msaada kwa sasa katika kikosi chao.

Wapo kina Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza, Henock Inonga na wengineo. Ina maana mwanzo wa msimu mpya ujao Simba itakuwa na kocha mpya, pia kundi kubwa la wachezaji wapya. Unaweza ukawa mwanzo mzuri kwa Simba ingawa kama tunavyoelewa wakati mwingine inakuwa ngumu kuunganisha timu kwa urahisi kama kila mtu anajikuta ni mpya kikosini.

Hata hivyo, hilo ni jambo ambalo mashabiki wa Simba wanatamani kuliona. Ili mradi tu wasajiliwe wachezaji wenye viwango hasa vya kuchezea Simba. Wasiwe kama hawa ambao wamesajiliwa katika madirisha machache yaliyopita. Wengi hawana hadhi ya kuchezea Simba.” — Edo Kumwembe

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

cc:Wasafi Fm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents