Michezo

Eng Hersi aeleza kwa upana njia ya Mafanikio ya Yanga SC

“Nimekabidhiwa Young Africans SC kama Rais nikiwa na miaka 37. Sio rahisi kijana mdogo kama mimi kukabidhiwa timu kongwe yenye miaka 89 na mafanikio makubwa. Tumepambana kuhakikisha wale waliokuwa wana fikra kuwa vijana hawawezi, wanabadili fikra hizo” Rais wa Young Africans SC

“Kwa sasa hakuna Klabu Tanzania inayoweza kuisogelea Young Africans SC kwenye ubora. Ndio maana timu nyingi zikicheza na sisi zinakuja na mfumo wa kuzuia zaidi ikimaanisha wanaiheshimu Klabu yetu. Malengo yangu makubwa ni kuhakikisha Klabu yetu inakuwa moja ya Klabu bora”
“Matamanio yangu ni kuona mwakani kwenye mashindano ya Kimataifa tufike katika orodha ya timu nne bora AFRIKA, ili tuweze kushiriki kombe la dunia la vilabu. Mwaka jana tumefika fainali na tumepata alama nyingi ambazo zitatuongezea nguvu ya kushiriki kombe hilo”
“Usajili ni sanaa, ni lazima ujue kwanini unafanya huo usajili. Kwa kifupi huwezi kubaki na Wachezaji wako wazuri kwa muda wote, hivyo inabidi utengeneze mazingira mazuri ya kuvutia Wachezaji wengine wazuri. Hivyo nilichukua maamuzi ya kusimamia mchakato wa usajili”
“Unapokuwa kiongozi lazima uwe na maono makubwa sana na uelewa mkubwa wa mpira. Unapaswa kujua mchezaji yupo kwenye kilele cha ubora wake, anapata wakati mgumu kuzuoea mazingira, amechoka nk. Usipokuwa na uelewa wa mpira basi utajikuta unasajili hovyo au unatimua wachezaji kwa hisia” Alisema Eng. Hersi
Imeandikwa na Mbanga B.
cc:BongoFm

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents