Burudani

Afande anatakiwa amwandikie mashairi Harmorapa – Majani

Producer mkongwe wa muziki kutoka Bongo Record, P-Funk  Majani  amemtaka rapa mkongwe Afande Sele kumuandikia mashahiri msanii Hamorapa anayechipukia kwenye game ili kutimiza ndoto zake na siyo kumkatisha tamaa.

Mtayarishaji huyo ambaye hivi karibuni alilitambulisha kundi lake jipya Bongo Los, amelazimika kumuomba Afande kufanya kazi hiyo baada ya kumdiss Harmorapa kwa kudai ”Harmorapa siyo msanii na hataweza kudumu kwenye ‘game’ ya bongo Fleva kwa muda mrefu”.

“Afande namuomba kitu , kama unaona dogo anayumba hutakiwi kumbeza bali unapaswa kumuandikia mashahiri na kukuza sanaa yake. Wewe ni Mfalme wa Rymes unapaswa kuwasaidia wadogo zako ambao wanaonyesha juhudi zao binafsi za kujituma. Siyo lazima Afande ufoke wewe usikike wasaidie hawa wachanga wainuke wawe bora kama wewe usiwakatishe tamaa ukiwa wewe ni kaka yao,” Majani alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio.

Aidha Majani ameongeza kwamba Harmorapa amebadilika kimuziki tofauti na alivyoanza hivyo ni vyema akazidi kupatiwa misaada mbalimbali ya kumkuza kipaji chake, huku akimwelezea ni kijana anayejituma, mwenye adabu, pia mwenye shauku ya kufika mbali kimuziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents