Burudani

Akon adai hajutii kuacha kumsainisha Drake kwenye label yake alipotambulishwa kwake mwaka 2005

Kama angemwelewa vyema, leo hii Drake angekuwa msanii wa Akon kupitia label yake ya Konvict Music, lakini hakushawishiwa na uwezo wake kipindi hicho.

Akon and Drake

Ilikuwa ni mwaka 2005 pindi rapper wa Canada, Kardinal Offishall alimpompelekea Akon nyimbo za Drake kuona kama anaweza kumchukua.

Hata hivyo Akon hakukikubali kipaji cha Drake kama alivyovutiwa na T-Pain na Lady Gaga pamoja na wengine aliowachukua.

Akiongea na TMZ, Akon amesema pamoja na hivyo hajutii kumuacha Drake ambaye kwa sasa amegeuka kuwa miongoni mwa rappers wenye mafanikio zaidi baada ya kusainishwa na Young Money.

“Hapana sijutii kabisa, muda ule nimemsikia Drake hakuwa kama alivyo leo,” alisema Akon. “Alikua kimuziki na kuwa msanii mzuri, kila mtu ana sehemu ya kuanzia na katika kipindi hicho hakuwa tayari kwa mtazamo wangu.”

Akon anasema kama angemsaini Drake haoni kama angefanya kitu tofauti na anachofanya sasa kwakuwa amechukua njia bora inayompa mafanikio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents