Bongo5 ExclusivesBurudaniHabari
Alikiba: Sina mawasiliano ya siri na Zuchu, napenda nyimbo zake
Siku ya jana wakati Alikiba anahojia kwenye kituo cha East Africa Radio aliulizwa kuhusu habari ilitrend kwa siku kadhaa kuwa ameshirikishwa na Davido kwenye album yake.
Alikiba alikanusha suala hilo na kuonya mitandao ya kijamii kwa kukuza vitu vya uongo, Alikiba aliongeza kuwa lini nimefanya ngoma na Davido, hata kama ingekuwa Davido angepost yeye.
Mbali na hilo muda mchache baada ya kutoka East Africa Redio alienda CloudsFm na wakati yupo kule kwenye XXL Alikiba amezungumzia ukaribu wake na Zuchu baada ya kuulizwa kuwa ana mawasiliano ya siri na Zuchu.
Alikiba alicheka kwanza halafu akajibu kuwa mara ya mwisho alionana na Zuchu Airpot na kusalimia naye tu ingawa anakubali yimbo zake na anapenda alivyo na nidhamu.