Habari

Askari wa kike wakabidhiwa bendera kwenda Abuja Nigeria

Kamishna wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi Nchini CP Awadhi Juma Haji amewakabidhi askari wa kike wa Jeshi la Polisi Bendera ya Taifa kwa ajili ya kuondoka nchini kwenda Nigeria kushiriki mafunzo ya askari wa kike Ukanda wa Afrika yanatarajiwa kufanyika Abuja Nchini humo kuanzia Julai 01 hadi tisa mwaka huu.

Akikabidhi bendera hiyo leo Makao makuu ndogo ya Jeshi hilo Jijini Dar es Salaam Kamishna Awadhi amewataka washiriki wa Mafunzo hayo kuzingatia nidhamu wakati wote wa mafunzo Abuja Nchini Nigeria ambayo yamelenga kuwajengea uwezo askari hao.

CP Awadhi ameongeza kuwa miongoni mwa mafunzo hayo ni Pamoja ni uongozi, afya ya akili na mafunzo mengine yanayohusu masuala ya ulinzi huku akibainisha kuwa mafunzo hayo yataleta tija kwa Jeshi la Polisi Nchini ambapo amewasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuzingatia mafunzo ambayo yatatolewa kuanzia Julai moja hadi tisa.

Aidha amewataka kuzingatia nidhamu ambapo amewasihi Kwenda kwao nchini Nigeria ni kuiwakilisha nchi huku akiwataka kuonyesha nidhamu ambayo italeta sifa kwa nchi na kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan.

Vilevile Kamishna Awadhi amewataka askari hao kutangaza sifa nzuri ya Tanzania ambayo imeenea kote duniani katika masuala ya amani na utulivu uliopo nchini huku akiwataka pia kuvitangaza vivutio vya Utalii vilivyopo hapa nchini.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents