HabariUncategorized

Atakaye dhibitika ni jangili, jambazi nitafuta uraia wake – Waziri Nchemba

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa inaweza kuwafutia uraia watanzania wapya waliopewa uraia wale ambao walikuwa wakimbizi wanaoishi makazi ya katumba Mishamo na Ulyankulu iwapo wataonekana kushindwa kufuata sheria za nchi na kujihusisha na vitendo vya uharifu na uvunjifu wa sheria za nchi,vitendo vya ubaguzi wenyewe kwa wenyewe ubaguzi wa kitabaka kubaguana kisiasa, kidini na kwa namna yeyote hawawezi kuvumiliwa hata kidogo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba wakati akiwahutubia raia hao wapya kwenye Makazi ya Katumba Halmashauri ya Nsimbo Wilayani Mpanda Mkoani Katavi wakati akiwataka kujiepusha na vitendo vya kubaguzi.

“Mimi najua uraia usiofutwa ni ule wa kuzaliwa mtu kama akishazaliwa kama ni Muafrika ata akiandikishwa kwingine anaendelea kuwa Muafrika. Lakini kama watu wanafanya vitu vya kinyama ambavyo hatujazoea na ubaguzi huo ndio uliosababisha matatizo kule hatuwezi tukaamisha matatizo kutoka kule tukayaishi tukiwa huku kama ugomvi kule ulizuka na watu wakakimbia yaliyogombana hayakuwa mabonde nama milima yalikuwa ni hao hao watu,” alisema Mwigulu.

“Kwahiyo ukianzisha ubonde na ummlima ukauhamishia hapa unaleta ugomvi ambao sisi hatukuuzoea kwa maana hiyo leo naongea kindugu kwa maana hiyo muonyane wenyewe kwa wenyewe ambiazaneni na mkimuona mtu yupo wa aina hiyo kwani nyinyi hamna wazee wambie hilo lina gharama hapa sio mahali pake, kwa bahati nzuri kamati ya ulinzi na usalama ipo hapa mtakapo muona mtu anafanya kaubaguzi wataweka mapendekezo na hamtajua ni saa ngapi wameweka kwahiyo kama mnapendana shaurianeni mapema sana hatutaki kusikia lugha za huyu anakaa juu anakaa bondeni hayatusaidii sisi hapa kwa yoyote atakae thibitika ni jangili,jambazi nitafuta uraia wake hatutampa muda wa kuchomoa chaji kwenye soketi tutamuondoa.”

Video:
https://youtu.be/fcLbUlgBCfE

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents