Burudani

Audio: Mez B aanzisha kampeni ya kuhamasisha watu kutulia kwenye mahusiano yao, atafanya ziara kwenye mikoa 5

Wakati kampeni maarufu ya ‘Baki Njia Kuu, Michepuko Sio Dili’ ikiendelea nchini kuwahimiza wanandoa kuwa waaminifu kwa wenzi wao, muimbaji wa Chamber Squad, Mez B ameanzisha kampeni yake kama hiyo.

MEZ-B-C

Akiongea kwenye kipindi cha Sunrise cha Times FM leo, Mez B amesema wazo la kampeni hiyo lilikuja baada ya kuachia wimbo wake uitwao ‘Shemeji’ unaozungumzia jinsi shemeji yake alivyoisaliti ndoa yake.

“Nimeona hili ni tatizo kubwa sana katika jamii yetu sasa hivi, watu wengi sana wanasaliti ndoa zao na mahusiano yao. Kwahiyo kwa kutumia nyimbo yangu nimeona nifanye kama kampeni ya kuhamasisha watu kutulia kwenye mahusiano yao,” amesema.

Mez B amesema katika kufanikisha hilo atazunguka katika mikoa mitano nchini ikiwemo Mtwara, Mbeya, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam na anatarajiwa kusindikizwa na wasanii wengine wakiwemo Afande Sele.

Msikilize zaidi hapa.

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/147517046″ params=”auto_play=false&hide_related=false&visual=true” width=”100%” height=”450″ iframe=”true” /]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents