Burudani

Audio ya ngoma yangu toka kwenye video isichezwe redioni tafadhali – Jay Moe

Rapper mkongwe aliyetikisa game kwa ngoma yake ya ‘Pesa Madafu’ Jay Moe amezuia redio kucheza ngoma yake mpya ‘Nisaidie Kushare’ kwasababu hajaachia bado audio yake rasmi.

“Nachoomba msiitumie audio mlioconvert kwenye video, audio wengi waliyo nayo ni ile walioconvert kwenye video ambayo sio sawa ina hadi zile sound za sms,” Moe amemuambia mtangazaji wa Ice Fm, Gami Dee.

Alipoulizwa kwanini ameamua kufanya hivyo kwa kuachia video tu, rapper huyo amesema, “Hii ni video yangu ya pili ndani ya miaka kibao iliyopita almost 11, kwahiyo ni kitu ambacho nilitamani siku moja nifanye kuona itasaidia kitu gani. Na kweli kama unavyozungumza naona imepokelewa vizuri.”

Jay Moe amesisitiza redio kusubiri mpaka official audio itakapotoka lakini wasitumie audio iliyo’convertiwa’ na bloggers.

Na Gami Dee
Instagram: @gamideetz
Email: [email protected]

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents