Burudani

Baghdad atahadharisha watu wasijekuelewa vibaya wimbo wake ujao ‘Ninae’, amewataja Diamond na Alikiba

Rapper Baghdad amewatahadharisha watu wasije kuuelewa vibaya wimbo wake ujao, ‘Ninae.’

20151002024851
Baghdad na mke wake

Rapper huyo ambaye alifunga ndoa July 25 mwaka huu na mchumba wake waliyedumu kwa miaka mitatu, ameiambia Bongo5 kuwa wimbo huo umefanyika kwenye studio za Kaburu Records na producer akiwa ni Islam Touches ‘Ninae’ unazungumzia mtu ambaye amepata mpenzi wa kuwa naye katika shida na raha.

Kwenye intro ya wimbo huo Baghdad anaeleza kuwa katika maisha ‘sio kile ulichho nacho bali yule uliye naye.’

Hata hivyo mstari mmoja uliopo kwenye wimbo huo umezua maswali mengi na amedai kuwa umekuwa sababu kubwa ya kuchelewesha kuutoa mpaka alipojiridhisha kuwaomba watu waliomzidi umri na wakongwe kwenye muziki wa Bongo Flava kuomba ushauri.

20151002025058

“Sio makafiri wanaopotosha umma kuwa Nasib kumuoa Ally sio ndoa batili,” unasema mstari huo. Baghdad anasema hakuwalenga wasanii hao kama watu wengi waliosikia na kudhani hivyo, bali anasema ilikuwa katika utundu wa kupanga vina.

Baghdad amesema watu wasije kudhani alikuwa akitaka kuchochea beaf kati ya Diamond na Alikiba.

Wimbo huo unatoka Jumamosi hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents