Habari

Bandari ya Dar Es Salaam yakanusha kuwa na Mgomo

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini TPA imekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kuhusu kudorora kwa utendaji kazi katika kuhudumia meli na shehena katika Bandari ya Dar es Salaam kulikohusishwa na mgomo wa wafanyakazi wenye madai mbalimbali ikiwemo kufutiwa mikataba yao ya kazi na kusema hakuna mgomo wala hujuma zozote bandarini hapo.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa hakuna mtumishi yeyote wa TPA aliyesitishiwa mkataba wake kwa sababu zozote zile na kwamba hata menejimenti ya mamlaka hiyo inatimiza ipasavyo jukumu lake la kusimamia kikamilifu utendaji wa idara ya vitengo vyote vya operesheni za kibandari katika Bandari ya Dar es Salaam kwa saa 24 ili kuhakikisha huduma zinatolewa kwa weledi, kasi na ufanisi wa hali ya juu. TPA imeongeza kuwa wote watakaobaini wanaohusika na kusambaza taarifa za upotoshaji juu ya Bandari ya Dar es Salaam watachukuliwa hatua kali za kisheria.

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

 

 

 

 

Chanzo; TPA TANZANIA

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents