Burudani

Barnaba ajiondoa kwenye mitandao ya kijamii

Msanii wa muziki ambaye pia ni producer wa High Table Sound, Barnaba Classic,  ameweka wazi kuwa ukimya wake utaanzia kwenye mitandao ya kijamii ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na kujipanga namna ya kuuanza kwa kishindo mwaka 2018.

“Nikiwa najitoa kwenye mitandao ya kijamii kidogo, ningependa kuwatakia mashabiki, marafiki na familia yangu Heri ya Christmas na Mwaka Mpya”, amefunguka Barnaba kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Pamoja na kujitoa kwake nyota huyo anayetemba na ngoma yake ya Mapenzi Jeneza ameongeza kuwa anajiweka vizuri kuanzia mwonekano mpaka sound ya hit zake zijazo.

“Ninapumzika kidogo ili kuweka mipango yangu vizuri kwaajili ya mwaka 2018. Nitawaletea Barnaba mpya mwenye kila jipya kimuziki na hata Sound” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents