Burudani

Barnaba asema mwaka 2014 atakuwa Mchamungu zaidi

Muimbaji wa THT, Barnaba Elias amesema mwaka 2014 atautumia kuwa karibu zaidi na Mungi ikiwa ni pamoja na kuanzisha taasisi yake kwaajili ya kusaidia watoto.

Barnaba-aki-smile-na-gitaa-lake

Barnaba ambaye ni Mkatoliki ameiambia Bongo5 kuwa kwakuwa Mungu amempa sauti nzuri ya kuwaimbia watu ni vyema akarudisha fadhila kwa ibada pamoja na kusaidia watoto na watu wasiojiweza.

“Wasichokijua kwa Barnaba mwaka huu ni mtu ambaye atakuwa sana mchamungu na mwenye kutoa sana kusaidia wanadamu, wananchi wenzangu wasiojiweza kama watoto yatima. Nadhani pia nitafungua foundation na hata kama sio foundation basi nitakuwa na NGO ambayo itatoa misaada midogo ambayo itaonekana ya sio kushawishiwa na mtu ni uamuzi wangu kufanya hivyo/. Pia nitakuwa tofauti sana mwaka huu nitafanya Bongo Flava ya Kitanzania bado lakini nahitaji kumuimbia Mungu mwaka huu,” amesema muimbaji huyo.

“Nastahili kufanya hivyo kwasababu kila kitu naamini mwenyezi Mungu ameshanipatia. Sauti nzuri na thamani ya muziki huu naofanya amenipatia. Imefika stage naamini kabisa natakiwa kufanya muziki wa Bongo flava pia na kukishawishi kizazi kinachofuata.”

Ameongeza kuwa hivi karibuni ataachia wimbo na video ‘Jasho la Mnyonge’ na kuwashauri wasanii wenzie wamrudie Mungu ili awarahisishe shughuli zao za muziki.

“Wasanii waache imani potofu wakifanya nyimbo zao. Hata kama zimebuma wanatakiwa kurudi kwa Mwenyezi Mung hata kama unafanya poa kwenye game lazima turudi kwa Mwenyezi Mungu ili atuongezee mafanikio zaidi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents