Burudani

BASATA ianze kukagua nyimbo kabla hazijatoka – Roma

Roma Mkatoliki amelishauri baraza la sanaa la taifa, BASATA kuunda kutengo cha kukagua nyimbo kabla hazijatoka.

roma new pic

Hivi karibuni baraza hilo liliufungia wimbo wake mpya, Viva Roma kwa madai una matusi na unatukana viongozi.

Roma ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa ili kwenda sawa na BASATA wanatakiwa kuunda chombo cha ukaguzi wa kazi za wasanii kabla hazijatoka.

“Nisiwe muongo, sijui taratibu zinazotumika ili kufikisha information zao kwa wasanii,” alisema. “Kwa sababu kitu ambacho naona ingekuwa rahisi kama artist kabla hajaachia nyimbo yake mpya ama hajafanya kazi yake ya sanaa, iwe inawasilishwa katika hicho chombo. Nadhani hapo tungekuwa tunaenda sawa,” aliongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents