Habari

BASATA watoa neno kufuatia taarifa za Ommy Dimpoz kurejeshwa Afrika Kusini kwa ajili ya matibabu

Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limetoa  neno kwa mara ya kwanza tangu siku ya jana taarifa zisambae mitandaoni kuwa msanii wa muziki nchini Tanzania, Ommy Dimpoz amerejeshwa Afrika Kusini alikokuwa akipatiwa matibabu.

Image result for BASATA OMMY DIMPOZ
Ommy Dimpoz

Taarifa ya BASATA hiyo ya BASATA imetoka yakiwa yamepita masaa 24 tangu kuenee kwa taarifa hiyo ya kuumwa tena kwa Ommy Dimpoz.

Imeripotiwa tena msanii na ndugu yetu @ommydimpoz amerejea hospitalini kwa matibabu zaidi. Tunasimama na wapenda sanaa, wapenzi wake na watanzania wote kwa ujumla katika kumwombea na hatimaye arejee katika afya yake. Tusimame naye katika dua na kumtakia kila kheri katika matibabu yake. #getwellsoon#ommydimpoz from #basata

Ommy Dimpoz tangu mwezi Mei amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya Koromeo ambayo yalipelekea afanyiwe upasuaji nchini Afrika Kusini ambako hadi leo bado anaendelea na matibabu.

Related Articles

10 Comments

  1. Basata nao kichwa maji jamani

    Sasa uongozi wa rockstar ushatoa tamko kuwa hali yake ipo vizuri alienda kwa chek up tuu basi kwa muujibu wa madaktar kila baada ya miezi mitatu alipoti

    Sasa nyie baraza eti mnatamka habari zinazoenea mtandaoni bila hata ya kuchunguza ivi baraza mpo serious kweli Jamani

    Nimeamini baraza wao wanakagua vya mtandaoni ndio mana kesi nyingi za baraza zinahusu wasanii kukaa uchi mitandaoni
    Mana hamuumizi bongo zenu kazk kufungia nyimbo tuu

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents