HabariMichezo

Battle ya msimu ya El Shehat na Yao Jeshi

Ukiacha ubora wa Yanga SC kwa Sasa ni ubora katika safi Yao ya ulinzi lakini hapa nataka kumgusia beki wa kulia wa Yanga Kouassi Ottoula Yao ‘Jeshi’ ambaye amekuwa katika kiwango Bora lakini ni beki ambaye anapenda kupanda kwenda kushambulia.

Bila shaka kwenye mchezo huu pia Yanga wataingia uwanjani kupambana kupata alama tatu muhimu hili kujiweka vyema pia lazima kutumia vyema uwanja wa Nyumbani kwa sababu kama hizo kocha wa Yanga upenda kuwapa majukumu beki wake kucheza juu kidogo lakini kwa bahati mbaya upande wa Yao Yao atakutana na Mtaalam fundi mchezaji ghali Afrika kuliko wote Hessein El Shehat akitokea ligi kuu ya Saudi Arabia kwa dau la billion 11 Moja kati ya wachezaji muhimu katika kikosi Cha Al Ahly.

Ni mchezaji mwenye Kasi anajua kukaa na Mpira uwezo wake wa kufanya maamuzi sahihi ni mkubwa ni msumbufu kwahiyo hili battle litakuwa la aina yake kwa beki wa Yanga kuhakikisha anasaidia kushambulia na muda huo huo El Shehat asifanye madhara katika lango lao.

Mtangazaji wa Mpira kutoka Azam Media @Hinjojr Amesema mechi ya Yanga SC na Al Ahly utakuwa mchezo mgumu kwa pande zote mbili lakini amesisitiza Al Ahly hawapo kwenye form Bora lakini wapo katika daraja lao la juu kama kawaida maana ndiyo level zao lakini kwa Yanga wapo kwenye kiwango Bora kwa Sasa na mechi za nyumbani kuanzia msimu uliopita wamepata matokea katika uwanja wa Nyumbani ivyo anawapanasilimia 50 ya kupata matokeo ya ushindi katika mchezo huo.

Credit by Isaya Dede

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents