Burudani

Batuli achukizwa na jinsi Kitale anavyosambaza picha za scene ya mapenzi kwenye filamu aliyoigiza na Stan Bakora

Wanasema ‘sex sells’ na ndio maana Kitale anatumia picha za scene ya mapenzi kati ya mshkaji wake Stan Bakora na muigizaji mrembo wa kike, Yobnesh Yussuf maarufu kama Batuli kutangaza filamu yake mpya.

11352159_1007925195905114_1155888978_n

Hata hivyo Batuli anahisi picha hizo zinamdhalilisha na amemtaka Kitale kuacha kuzitumia mara moja.

“Kwanza mniwie radhi watanzania mnachokiona na kinachoelezewa ni vitu viwili tofauti mwenye akili timamu anapata jibu kamili,” ameandika kwenye Instagram.

“@mkudesimbaoriginal nikuulize hivi wakati unampa @matejamusa picha ulimwambia ni za nn!? Hivi naweza kuwa faragha mbele ya camera!? Hata kama unapromote movie hii sio kihivyo kama kupromote kitu ndio hivi basi fani yetu imejaa mazumbukuku. Hii ni scene iliyopo kwenye movie sioni sababu ya kunichafua kijinga hivi, kizuri kinajiuza @mkudesimbaoriginal kuandika shit sio njia sahihi ya kupromote kazi yako,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents