Burudani

Ben Pol akiri watu wengi waliiona Jikubali ni ya kawaida kabla ya video, ‘video imeiongezea thamani Jikubali’’

Mshindi wa KTMA 2013 katika kipengele cha mtunzi bora wa mashairi ya Bongo Flava, Ben Pol amesema watu wengi waliichukulia poa ngoma yake mpya Jikubali kabla hajatoa video yake.

Amesema msiba wa Ngwair ulikuwa ni sababu nyingine Jikubali iliathirika na kushindwa kuingia vizuri kwenye masikio ya watu kwakuwa radio nyingi zilijikita kupiga nyimbo za Ngwair na za kuomboleza zaidi.

“Nakubali kabisa kwamba mwanzo ilipotoka ni kweli kulikuwa na ukawaida fulani halafu plus na msiba, rotation ya nyimbo nyingi mpya zikapotea kwahiyo kwa nyimbo kama Jikubali ambayo watu waliichukulia easy easy na yenyewe ikawa moja wapi zilizowekwa pembeni ya muziki uliokuwa unalia katika wiki na nusu ile ya msiba,” amesema Ben Pol.

“Kwahiyo hii video imekuja imeboost na vile vile ni kali, Nisher amefanya kazi kubwa na nimejaribu pia kufanya hisia kwenye video, watu wameanza kuconcentrate kwenye neno hadi neno.”

Kwa upande wake Lucci aliyetengeneza wimbo huo amesema hata kabla ya video alikuwa anajua jinsi Jikubali ulivyo wimbo mkubwa. Mpaka sasa video ya Jikubali imeangaliwa kwa zaidi ya mara 17,000 kwenye You Tube tangu iwekwe June 10.

Wasikilize zaidi wote hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents