Habari

Benki ya CRDB, NALA kuwapa Diaspora urahisi wa Kutuma Fedha Nyumbani

 

Benki ya CRDB leo imetangaza ushirikiano na kampuni ya Nala kuwawezesha Watanzania waishio nje ya nchi ‘Diaspora’ kutuma fedha nchini kwa gharama nafuu, usalama na urahisi.

 

Ushirikiano huo umetangazwa katika hafla fupi iliyofanyika katika Makao Makuu ya Benki hiyo ambapo Mkurugenzi wa Wateja Wadogo na wa Awali wa Benki ya CRDB, Bonaventura Paul na Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa NALA, Benjamin Fernandes walisaini mkataba wa ushirikiano.

Akizungumza katika hafla hiyo Bonaventura amesema ushirikiano huo na NALA ni mwendelezo wa jitihada za Benki ya CRDB katika kurahisisha huduma kwa diaspora wa Tanzania.

Kwa upande wake, Fernandes amesema kati ya changamoto zilizopo kwa diaspora ni gharama kubwa za kutuma fedha nyumbani. Amesema ushirikiano huo na Benki ya CRDB utawawezesha diaspora kutoka mataifa 29 duniani ambapo NALA inatoa huduma kutuma fedha nyumbani.

Ushirikiano huu unawezesha pia unakwenda kurahisha upokeaji fedha kutoka nje bila gharama kwa wateja wa taasisi zote za fedha ambapo Benki hiyo itakuwa ikichakata miamala yote inayotumwa kupitia NALA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents