Burudani

Billion akaa studio miaka 15 akiwasaidia mastaa kuingiza sauti, kuwarekebishia mashairi

MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Abdallah Manyuti maarufu kama Billion amefunguka na kusema kuwa amekaa studio kwa mtayarishaji wa muziki Sheddy Clever zaidi ya miaka 15 akifanya kazi ya kuwasaidia mastaa kuingiza sauti na kuwarekebishia mashairi.

Billion aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Bongo5 kuhusu safari yake ya muziki na namna alivyojipanga kuwa burudisha watanzania kupitia nyimbo.

Anasema nyimbo ambazo ameshiriki kwa asilimia kubwa katika utengenezaji na kutoa mawazo ni Number One ya msanii Nasibu Abdul maarufu Diamond Platinumz, Merry You ya Richmavoko, Zilipendwa ya Matonya pamoja na Nivute Kwako ya Dayana Nyange.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Abdallah Manyuti maarufu kama Billion

Aidha anasema ameanza muziki tangu mwaka 2003 lakini 2014 ndiyo alitoa wimbo wa kwanza uliyojulikana kwa jina la ‘Tamutamu’ lakini haukufanya vizuri na mwaka 2018 alitoa nyimbo zingine mbili nazo hazikufanya vizuri.
“Mwaka 2024 nimerudi rasmi na kutoa wimbo wangu wa kwanza unaitwa ‘Ajue’ ambao umefanywa na mtayarishaji wa muziki Sheddy Clever ninaimani utafanya vizuri, hata hivyo tayari nimesharekodi nyimbo 108,” alisema na kuongeza

“Asilimia 100 nyimbo zangu naandika mwenyewe na nimeshawaandikia wasanii wengi wakubwa nyimbo mbalimbali ambazo zinafanya vizuri hapa nchini,” anasema Billion

Hata hivyo anasema anawaomba mashabiki wake na watanzania kwa ujumla wamsapoti kwani menejimenti yyake imejipanga vizuri hasa kuleta maajabu kwani wana nyimbo kali na zenye kuvutia.

“Kiu yangu ni kufika mbali kimuziki na ili nifanikiwe naomba kupata sapoti kutoka kwa watanzania, muziki unathamanikubwa kwani tunawaona Diamond, Harmonize, Alikiba, Rayvanny, Marioo wote hawa wanavipaji na wanatengeneza fedha nyingi kupitia muziki,” anasema Billion

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents