Burudani

Birthday Gift: Beyonce amnunulia Jay-Z saa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6!

Jay-Z apewe nini kingine zaidi ya mke ampendaye kama Beyonce? Inadaiwa kuwa Beyonce amemzawadia kwa surprise mume wake huyo saa yenye thamani ya dola milioni 5 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 6 za kitanzania.

Zawadi hiyo ni ya birthday ambayo Jay-Z husherehekea kila December 4.

Saa hiyo iliyotengenezwa kwa almas ni aina ya HublotBig Bang – saa ya mkononi yenye gharama zaidi duniani.

Kampuniya kifaransa inayotengeneza saa hizo, LVMH, imedai kuwa huchukua watu 17 na miezi 14 kubuni na kutengeneza saa kama hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa Beyonce kumzawadia mumewe zawadi aghali kwani mwaka jana alimzawadia gari aina ya Bugatti yenye thamani ya Euro milioni 1.8.

Si ajabu kwa Beyonce kumwaga hela kiasi hicho kwani kwa mwaka huu pekee ameingiza Euro milioni 32 kutokana na muziki na biashara zake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents