Burudani

Bizman amtaka Mr Ttouch, Laizer na maproducer wengine kujiongeza

Msanii na mtayarishaji mkongwe wa nyimbo za BongoFleva, Bizimana Emmanuel aka Bizman amewataka watayarishaji wapya wa muziki akiwemo Mr Ttouch kutoka Touchz Sound, Laizer wa WCB Record pamoja na watayarishaji wengine kuongeza vionjo kwenye beat zao wanazoandaa.

Muimbaji huyo ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo Nipe Muda, Ametoroshwa,  Mabinti wa Bongo na nyingine nyingi, amesema wako wandaaji wa muziki wanaofanya vizuri huku akiwatolea mfano, Laizer wa WCB na Mr Ttouch lakini akiwataka kuongeza vionjo kwenye kazi zao.

“Wako wandaaji wanaofanya vizuri kama Mr Ttouchez Laizer na wengine lakini waongeze juhudi na wajifunze kutumia vifaa vingi zaidi vya muziki” alisema Bizman.

Alisema watayarishaji wa muziki wana nafasi kubwa na kuufanya muziki huo kuwa nzuri na tofauti na ule ambao wanapatikana duniani kote.

Katika hatua nyingine mtayarishaji huyo amekipinga kitendo cha wasanii kunya pombe ili wapate mzuka wa kwenda kurekodi.

“Msanii kurekodi nyimbo kipande kipande kunaweza kumjenga au kumbomoa , wasanii wengi wanatumia pombe au kilevi kingine wakiamini Inatawapa morali wa kurekodi kumbe ndo wanaharibu kabisa” alisema Bizman.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents