Burudani

Bob Junior azungumzia kuchelewa kwa kolabo yake na Chameleone, pamoja na ujio wa album ya ‘Ukweli Wangu’

Mwanamuziki na producer wa Sharobaro Records, Bob Junior amezungumzia sababu ya kuchelewa kwa kolabo yake na nyota wa Uganda, Jose Chameleone pamoja na ujio wa album yake iitwayo ‘Ukweli Wangu’.

Bob Junior Sharobaro
Bob Junior

Akizungumza na Bongo5 leo, Bob Junior alisema sababu kubwa iliyosababisha kuchelewa kutoka kwa wimbo huo, ni Chameleone kuwa busy sana na kushindwa kukaa pamoja na kufanya video.

“Huu wimbo umerekodiwa Tanzania na Kenya, na ninayo tayari lakini hatukutaka utoke bila video, audio ninayo muda sana, sasa hivi hata mwezi wa tatu ninayo. Tumefanya Sharobaro Records na Uganda pamoja tumeshirikiana, kwahiyo tukaona kwamba nikitoa audio peke yake sawa inaweza ikafanya vizuri lakini tulihisi ikitoka kwa pamoja audio na video itakuwa ni vizuri zaidi ili watu waone tupo serious kiasi gani. Kwahiyo video tupo kwenye process ya kufanya, Chameleone amependekeza tufanyie hapa Tanzania kwahiyo nimeshamtumia baadhi ya video za directors wa Tanzania aangalie halafu atachagua tufanye na nani, kwahiyo najua mashabiki wanasubiri kwa hamu lakini ukweli ni kwamba ngoma itatoka baada ya kumalizika kwa video,” amesema Bob Junior.

DSC_4614

Katika hatua nyingine Bob Junior amezungumzia ujio wa album yake mpya ‘Ukweli Wangu’ yenye nyimbo nane.

“Nina album ina nyimbo nane ambazo zipo tayari na nipo kwenye mipango ya kuangalia jinsi gani nitaitoa kati ya mwezi wa pili au wa tatu, album inaitwa Ukweli Wangu, nina studio na ninarekodi mwenyewe nikaona watu wanahitaji nyimbo nyingi kutoka kwangu kwanini nisiwape? Nimeona kuna kila sababu ya kutoa albam ya kuwapa mashabiki wangu kazi nyingi kwa pamoja, kwahiyo soon album itakuwa mtaani,” alisema Bob Junior.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents