Habari

Bobi Wine anunua boti la thamani ya $750,000

Wasanii wa Uganda wanasifika kwa maisha ya kushow-off. Kuanzia magari wanayomiliki, mijengo wanayoangusha na sasa hadi kwenye kumiliki private boats.
Msanii wa kwanza kufanya hivyo ni Bobi Wine ambaye hivi karibuni amenunua private boat yenye thamani ya dola za kimarekani 750,000.
Pamoja na gharama hizo za kuinunua, Bobi Wine ameilipia kodi boti hiyo inayofikia shilingi milioni 175 za Uganda.
Hata hivyo mpinzani wake wa siku nyingi Bebe Cool amemponda Bobi Wine kwa kusema kuwa anajisifia wakati boti sio ya kwake.
Bebe anasema Bobi ameshindwa kuimba hivyo anatafuta umaarufu kwa kudanganya kumiliki vitu visivyo vyake.
Anasema anamfahamu Bobi vizuri na hana uwezo wa kununua boti yenye gharama kubwa kiasi hicho.
Hata hivyo Bobi ameendelea kusisitiza kuwa hiyo ni boti yake aliyoinunua Miami, Florida nchini Marekani na ameipa jina la ‘Regal Sport Yacht’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents