Burudani

Bondia Frank Bruno apanga kurejea ulingoni akiwa na miaka 54

Bondia wa Uiengereza, Frank Bruno ametangaza huenda akarejea tena ulingoni.

Ametangaza uamuzi huo kwenye mahojiano na kituo cha runinga cha ITV. Hata hivyo mashabiki wa ndondi wameonesha wasiwasi na afya yake.

Bondia huyo ambaye amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili kwa miaka mingi, amesema hana namna lakini kuendelea na ndondi tena licha ya umri kumtupa mkono na kwamba amekuwa akifanya mazoezi kila siku na bado yuko gado.

Wataalam wa ndondi hata hivyo wameonya kuwa si vyema kama akirejea tena ulingoni. Bruno aliwahi kuwa bingwa wa dunia na mapambano yake na Tyson yalimpatia umaarufu licha ya kushindwa yote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents