Bongo MovieBurudani

Bongo Movie ina wakati mgumu sana – JB

Msanii mkongwe wa filamu, Jacob Stephan ‘JB’ amefunguka kuzungumzia sakata linaloendelea kuhusu kupigwa ‘STOP,’ filamu ‘feki’ za nje kwa manufaa ya soko la filamu za ndani.

Hatua hiyo imekuja baada hivi karibuni baadhi ya wasanii wa filamu kuandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, kupiga vita filamu feki za nje ambazo hazilipi kodi, kwa madai vinaliharibia soko filamu za ndani ambazo zinalipa kodi.

Baadhi ya wasanii pamoja na wadau wa filamu nchini wamekuwa wakiipinga hatua hiyo kwa madai soko la filamu limeharibiwa na kazi mbovu za wasanii.

Akiongea na waandishi weekend hii, JB amesema wao kama wasanii wameona ni sahihi kuzuia filamu za nje kwa kuwa hazilipi kodi huku akidai serikali ilishindwa kuzipiga vita na wao watagoma kulipa kodi.

“Bongo Movie sasa hivi iko katika wakati mgumu sana, waigizaji wengi sasa hivi hawaigizi kwanini  kulikuwa na vita ya wasambazaji, msambazaji wetu (Steps)  alikuwa ameshindwa kufanya kazi na hawa wafanyabishara,” alisema JB. “Hawa wafanyabishara wa CD ‘feki’ za nje walikuwa wanauza kazi zetu na kusambaza sasa baada ya kutokubaliana kibiashara na Steps, wakaanza kuuza kazi za nje nikisema hivi watu hawata nielewa,”

Aliongeza, “Tunakubali kwamba filamu za nje zilikuwa toka mwanzo lakini hazikuwa nyingi hivi ndio maana nasema haya maduka yalibadilika kutoka kwenye Bongo Movie kwenda kwenye filamu za nje. Kwa hiyo sisi siyo kwamba hatutaki filamu za nje hapana, tunataka zifuate taratibu kama ambazo tunafuata sisi, sisi kila filamu ambayo tunauza tunalipa asilimia 30 ya kile tunachokipata kama kodi lakini wao wahalipi ndiyo maana hata wanauwezo wa kuuza filamu zao shilingi 800 mpaka 1000 kwa sababu hawatumii gharama yoyote. Tunavyolalamika nia yetu ni kukuza tasnia ya filamu kwenda mbele zaidi, mimi nimebakiza filamu moja nistaafu kwa hiyo sifanyi hii movement kwaajili yangu ni kwajili ya watu ambao wanakuja,”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents