Habari

Bonta kuhusu matokeo ya form 4: Serikali imechagua quantitative na sio qualitative education

Rapper wa Arusha ambaye pia ni daktari wa binadamu, Bonta aka Maarifa amesema matokeo ya kidato cha nne mwaka huu ni mabovu kwakuwa serikali imechagua kuwa na shule nyingi badala ya kuzingatia ubora wa elimu.
bonta
“Serikali yetu imechagua mfumo wa quantitative education na sio qualitative, yaani wanazingatia zaidi kuwa na shule nyingi ambayo ndio quantity lakini hawaangalii quality za hizo shule, ni sawa sawa na kuchukua sukari kijiko kimoja ukajaza chai katika pipa halafu ukakoroga ile sukari,” anasema Bonta.

Amesema ubora wa elimu ya Tanzania umekuwa mdogo ukilinganisha na wanafunzi wanaomaliza ambao ni wengi.

“Hiyo namba asilimia kuwa ya waliofeli inaonekana kubwa kwasababu watu wametoka wengi katika shule za kata. Huwezi ukamfananisha mwanafunzi anayesoma Feza Boys pale na mwanafunzi ambaye anayesoma labda shule ya kata ya Isaka, sababu kule unakuta wana walimu zaidi ya ishirini, hapa kuna walimu wanne, walimu wanne hao kwa mwezi wa siku 30 wanaweza wakafundisa hata siku 20 maake kuna weekend, mwalimu huyu kafuata mshahara mjini mbali atakaa siku mbili tatu atarudi, hakuna maabara, hakuna vitabu,”

Bonta ameongeza kuwa miaka ya hivi karibuni elimu imekuwa ghali na hivyo kugeuka kuwa kama bidhaa.

“Elimu imekuwa ni commodity, elimu imekuwa ni bidhaa kama sukari, mtu mwenye hela ndio anakunywa chai yenye sukari, mtu ambaye hana sukari anakunywa chai ambayo haina sukari, ada imekuwa kubwa kiasi kwamba mtu unalipa ada utadhani unataka kununua shule. Utagundua kuwa wanaosoma ni matajiri, maskini sisi tunafuta ujinga tu,” anasema Bonta.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents