Burudani

Bushoke awakusanya Jaydee na Mandojo na Domokaya kwenye nyimbo zake mbili

Bushoke amejipanga kuja na kolabo mbili tofauti, moja akiwa na Lady Jaydee na nyingine akiwa na Mandojo na Domokaya ili kupata ladha tofauti ya muziki wake.

bushoke

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Bushoke alisema katika kuangalia nani afanye naye kolabo anaangalia kitu cha ziada alichonacho msanii.

“Nina nyimbo ambayo nataka nimshirikishe Mandojo na Domokaya japo wapo kimya kwenye game. Hiyo nyimbo niliyotunga naiona haiwezi kumfaa mtu yeyote isipokuwa Mandojo na Domokaya. Pia nina nyimbo ambayo nataka kumshirikisha Lady Jaydee,” alisema.

“Kwahiyo wanamuziki wapo wengi lakini mimi naangalia kitu cha ziada. Sinaga wazo labda nimtumie msanii kama Alikiba au Diamond ili nipate kiki ya kurudi, sinaga hizo toka zamani mimi nina muziki wangu ambao unajitegemea,” alisisitiza.

Pamoja na wasanii hao, Bushoke amesema atakuwa na kolabo za kimataifa pia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents