Habari

Bwana harusi apigwa risasi sehemu za siri katikati ya sherehe ya harusi yake

Bwana harusi nchini Misri amejeruhuwa vibaya kwa kupigwa risasi katikati ya sherehe ya harusi yake.

Bwana harusi huyo aliyetambulika kwa jina la Osman al-Alsaied alipata majeraha mabaya katika sehemu yake ya siri, Kiunoni na Mkononi katikati ya sherehe ya harusi yake ambapo mtu huyo aliyempiga alikuwa anafyatua risasi kama kitendo cha kusherehekea harusi hiyo .

Osman al-Alsaied (28) alikuwa akisherehekea harusi yake ndipo mwanaume mmoja alikosea kufyatua risasi badala ya kuelekeza juu silaha hiyo yeye alielekeza chini na kumjeruhi bwana harusi.

Maafisa wa polisi mjini Cairo wamethibitisha taarifa hizo kwa kusema kuwa bunduki hiyo ilifyatuliwa mwananume mwenye umri wa miaka 26 .

Hata hivyo, PolisiĀ  wamesema kuwa mtuhumiwa huyo aliyefyatua risasi alikamatwa na kuhojiwa muda mfupi baada ya tukio hilo kutokea.

Tukio hilo limeibua mijadala mingi kwenye mitandao ya kijamii nchini Misri wengi wakitaka tamaduni hiyo ifutiliwe mbali.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mtandao wa BBC zimeeleza kuwa bwana harusi huyo anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo na tukio hilo limetokea wiki iliyopita.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents