Burudani

BASATA wapokea nakala ya barua ya Msondo kuidai WCB milioni 300

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekiri kupokea nakala ya barua kutoka Bendi ya Msongo Ngoma kupitia kampuni ya sheria ya Maxim Advocates ikiitaka kampuni ya WCB inayomilikiwa na Diamond kuilipa bendi hiyo milioni 300.

Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza na Rais wa WCB, Diamond

Kampuni hiyo ya sheria imedai WCB walitumia kionjo cha melody ya saxaphone cha wimbo wa bendi hiyo bila hurusa katika wimbo wa WCB uitwao ‘Zilipendwa’.

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Katibu Mtendaji wa BASATA Godfrey Mngereza amesema wao wamepokea nakala ya barua hiyo ambayo inaitaka kampuni ya WCB kuilipa bendi ya Msongo Ngoma fidia ya milioni 300 kutokana na kutumia kionjo cha wimbo wao.

“Ni kweli sisi tumepokea nakala ya barua ambayo inaonyesha Bendi ya Msondo Ngoma inataka kulipwa milioni 300 kutokana na kutumiwa kionjo chao cha wimbo bila makubaliano,” alisema  Godfrey Mngereza.

Aliongeza, “Sisi hatuna chakusema kwa sababu kila msanii ana haki ya kudai haki yake kama anaona kuna namna mtu au kikundi kimetumia kazi yake bila makubaliano, tena hili suala lipo kisheria zaidi kwahiyo kungeacha sheria ifanye kazi yake,”

Bongo5 bado inafanya jitihada za kumtafuta mwanasheria wa Msondo Ngoma pamoja na COSOTA ili wachanganue jinsi kiasi hicho cha pesa walivyokikokotoa.

Hata hivyo WCB hawajatoa taarifa yoyote kuhusu sakata hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents