Habari

Watu 11 wafariki dunia baada ya mtambo wa Kiwanda cha Mtibwa Sugar kupata hitilafu

Watu 11 wamefariki Dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada kutokea kwa hitilafu kwenye mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme katika Kiwanda cha kuzalisha Sukari Mtibwa Sugar kilichopo Tuliani Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shabani Marugojo amesema tukio hilo limetokea saa 7:30 Usiku kuamkia leo Mei 23, 2024.

“Kulitokea hitilafu katika mtambo wa mvuke wa kuzalisha umeme kwenye kiwanda cha hicho na kusababisha vifo vya watu 11 ambao walikuwa kwenye chumba za kudhibiti mitambo hiyo,” amesema.

Kamanda amesema kati ya waliofariki kuna raia watatu wa kigeni kutoka Kenya, India na Brazil ambapo miili ya wote waliopoteza maisha imehifadhiwa Hospitali ya Mtibwa Sugar huku majeruhi wawili wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Misheni ya Bwagala.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents