Habari

Mambo 10 ya serikali kuhusu udahili na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu

Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na teknolojia imetoa kauli kuhusu udahili na utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka 2017/18 iliyotolewa na Prof. Ndalichako bungeni Mjini Dodoma. Ambapo udahili wa wanafunzi waliioomba kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ulifanyika kwa awamu tatu ulihusisha jumla ya vyuo na taasisi za elimu ya juu 67.

Prof Ndalichako alitoa kauli hiyo jana ambapo alitoa na changamoto zilizojitokeza Katika Utoaji wa Mikopo.

#Udahili wa wanafunzi walioomba kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ulifanyika kwa awamu tatu na ulihusisha jumla ya vyuo na taasisi za elimu ya juu 67.

#Katika awamu ya kwanza majina 77,756 yakipokelewa TCU, wanafunzi 44,627 walichaguliwa.

#Baada ya uhakiki waombaji 36,831 waliidhinishwa na kujiunga na shahada ya kwanza. Waombaji 7,796 walikuwa na kasoro mbalimbali kwenye taarifa zao hivyo kukosa sifa ya kujiunga na vyuo.

#Awamu ya pili ililenga waombaji waliokosa udahili awamu ya kwanza ambapo jumla ya waombaji 19,488 walijitokeza na walioidhinishwa kuwa na sifa za kujiunga ni 9,525.

#Awamu ya tatu ilikuwa kwa ajili ya kutoa nafasi ya mwisho kwa wanafunzi waliokosa vyuo ambapo jumla ya waombaji 7,418 waliidhinishwa kujiunga na vyuo.

#Hadi kukamilika kwa awamu ya tatu waombaji 63,737 waliidhinishwa kujiunga na vyuo na waombaji 28,466 kati yao walikuwa wamechaguliwa zaidi ya chuo kimoja.

#Serikali katika mwaka wa fedha 2017/18 imepanga kutumia Shilingi Bilioni 427.54 kugharamia mikopo kwa ajili ya wanafunzi wenye uhitaji na waliodahiliwa na vyuo vya elimu juu hapa nchini.

#Mikopo hii ni kwa ajili ya wanafunzi 122,623 ambapo wanafunzi 30,000 ni wa mwaka wa kwanza na wanafunzi 92,623 ni wanaoendelea na masoma.

#Katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa masomo, Wizara imepokea Shilingi Bilioni 147.06 kwa ajili ya ada za wanafunzi na kwa ajili ya kugharamia chakula, malazi, vitabu, viandikia na mahitaji maalum ya masomo.

#Utoaji wa mikopo umezingatia vigezo vilivyowekwa ambavyo ni ulemavu, uyatima na uhitaji hasa katika programu za kipaumbele.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents