Burudani

Chidi Benz adai kamwe hatomsamehe Baghdad kwa kitendo alichomfanyia

Matumaini ya rapper Baghdad kusamehewa na Chidi Benz kwa kitendo chake cha kuwashirikisha pamoja na Nay wa Mitego kwenye wimbo mmoja bila ya kuwapa taarifa, yamezimwa rasmi baada ya Chidi Benz leo kusema ‘kamwe hawezi kumsamehe.

12
Baghdad akiwa na warembo wakati akishoot video ya wimbo huo ‘Waambie Nipo’ aliowashirikisha Nay wa Mitego na Chidi Benz

Chidi ambaye yupo jijini Nairobi Kenya, alikuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Mambo Mseto cha Radio Citizen.

Akimuita Baghdad ‘Mpu**avu Chidi anasema alichukizwa mno na kitendo hicho kwakuwa siku anakwenda kurekodi verse yake alikuwa ana show Tegeta lakini aliamua kuchelewa kwenda ili kutimiza ombi la Baghdad.

Amesema Baghdad amemsumbua kwa siku nyingi akitaka afanye naye collabo na amwelezea kuwa hata wasanii wengine wanamjua kuwa ni ‘mjinga mjinga’.

Kwa upande mwingone akimzungumzia Nay wa Mitego, Chidi amesema hamjui na wala hataki kumsikia huku akisema kuwa siku akifikia level za wasanii kama Young D ama Nyandu Tozi ndio anaweza kumwelewa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents