Burudani
Trending

Dansa wa WCB Angel Nyigu afunguka: Kufanya kazi na Diamond ni ngumu sana (Video)

Bongo5TV imefanya mahojiano na dansa wa kike @angelnyigu ambaye anafanya kazi WCB, ambapo amefunguka kuhusu maisha yake binafsi pamoja na jinsi anavyofanya kazi na @diamondplatnumz .

Angel Nyigu ambaye kwa sasa ni mmoja kati ya dansa wa kike mwenye mafanikio zaidi kwenye kazi zao nchini Tanzania, amedai wakati anaanza kazi hiyo alitoroka nyumbani kwa walezi wake baada ya kukataliwa kufanya anachokifanya

Nyigu ambaye kwa sasa ana wafuasi zaidi ya 700,000 kupitia mtandao wa Instagram na kumfanya kuwa dansa wa kike mwenye followers wengi Tanzania, amefungua darasa la dancing Mwenye jijini Dar Es Salaam ambapo kwa sasa anapokea zaidi ya vijana 40 kwa wiki ambao wanataka kujifunza.

Pia dansa huyo kwa sasa ana channel yake ya YouTube ‘Angel Nyigu’ yenye subscribers 76000 ambayo anaitumia kwaajili ya kuweka matukio yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents