Burudani

Dar tujivunie kumpata RC mwenye akili nyingi – Wema Sepetu

Malkia wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu ameonyesha kuguswa na utendaji mzuri wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Wema na RC Makonda

Muigizaji huyo toka arejee Chama Cha Mapinduzi (CCM) akitokea CHADEMA, amekuwa karibu zaidi na mkuu huyo wa mkoa.

Alhamisi hii Wema amepost picha ya mkuu huyo na kuandika ujumbe unaowataka wakazi wa Dar es salaam kujivunia mkuu huyo kutokana na utendaji wake wa kazi.

“Tanzania Kwanza. Katika vitu ambavyo Dar pia inatakiwa kujivunia ni kupata RC mwenye akili nyingi… Mungu akakutangulie katika kazi zako za lengo la kuijenga Tanzania yako izidi kuwa zaidi ya ilipo sasa,” aliandika Wema.

Aliongeza, “Ipo siku wataelewa tu, The Man Himself… Call Him Mr Dar-es-salaam… Viva RC wangu…. Viva Rais wangu…. #UzalendoKwanza … cc @paulmakonda May everything you wish well for your Nation Be…. We support you fully,”

Muigizaji huyo bado anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya baada ya kudaiwa kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake kupitia kampeni ya kupambana na dawa za kulevya iliyoanzishwa na RC Makonda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents