Habari

Dar: Watu 7 mbaroni kuteka na kudai Bil. 8.7 kwa wazazi ili wamuachie binti yao (Video)

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata watuhumiwa 7 kwa tuhuma za kupanga njama, kumtishia kwa silaha, na baadae kumteka mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hani Nooh Hussein (29) Mkazi wa Masaki, Dar es Salaam.

Tukio hili limetokea tarehe 16 Oktoba 2023 majira ya saa nne asubuhi wakati Bi. Hani Nooh Hussein akiwa anaendesha gari lake namba T.333 CHN Toyota Rav4, ghafla akiwa eneo la Msasani Village alisimamishwa na sehemu ya kundi la watuhumiwa hao na kuingia ndani ya gari, kumtishia kwa silaha, kumteka na kuelekea maeneo ya Mbezi beach mtaa wa ujirani ambako walimshikilia kwa nguvu kwa siku nne huku wakidai pesa kwa vitisho kwa baba wa mhanga kuwa asipotoa kiasi cha dola za kimarekani milioni 3.5 mtoto wake atapotezewa maisha.
Jeshi la Polisi mara baada ya kupata taarifa ya tukio hilo lilifanya kazi ya ziada ya ufuatiliaji wa kisayansi na tarehe 19 Oktoba 2023 Jeshi la Polisi lilifanikiwa kumuokoa mhanga na kuwakamata watekaji wote wakiwa na gari walilomteka nalo pia silaha iliyotumika Pistol Glock 19 yenye namba LZB 614 iliyotengenezwa Austria ikiwa na risasi 4 silaha, na baadae kumteka mwanamke aliyefahamika kwa jina la Hani Nooh Hussein (29) Mkazi wa Masaki, Dar es Salaam.

Watuhumiwa waliokamatwa ni 1. Hassan AbusherNur (39) Raia wa Canada mwenye asili ya Somalia, Mkazi wa Msasani, 2. Nathan Lungumisa (27), 3. Fredick Chahonza (49), 4. Assad Abdurasur (43), 5. Fahad Mussa (32), 6. Ilfan Saleh (41), 7. Nicolas Nilay (39).

Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa tukio hili na leo tarehe 30 Oktoba 2023 watuhumiwa wote watafikishwa mahakama ya Kisutu kwa hatua zaidi za kisheria.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kutoa onyo na kuwa halitosita kuchukua hatua za haraka kwa mtu au kundi lolote linalopanga au kujihusisha na vitendo vya kihalifu. Jeshi lina waomba wananchi kuendelea kuchukia uhalifu na kutoa taarifa za wahalifu kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi haraka kabla ya matukio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents