Burudani

Davido na Wizkid waonyesheana Chuki

Wasanii wawili wakubwa wa muziki nchini Nigeria Wizkid na Davido ‘waliwasha moto’ katika mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumatatu baada ya kutupiana cheche za maneno.

Waimbaji hao wawili wenye mamilioni ya wafuasi duniani kote wanachukuliwa kuwa wapinzani huku wapenzi wengi wa muziki wa Nigeria wakijiweka kama “Team Wizkid” au “Team Davido”.

Mzozo huo ulizuka baada ya mashabiki kumtaka Wizkid kuwaachia wimbo mpya kwenye X. Alijibu kwa kuweka video yenye utata ya Davido na kuandika “niombe hivi, nitume video”.

Miezi kadhaa iliyopita video yenye utata ya mtu anayefanana na Davido ilisambaa mitandaoni ambapo alionekana akiomba mtu amsaidie.

Davido, 31, alijibu kwa kusema hatapoteza muda na juhudi zake kwa mtu ambaye kazi yake ilifufuka miaka michache iliyopita kabla ya kufa tena kama jibu la chapisho la Wizkid.

Vita vya maneno vimevutia hisia nyingi kwenye mitandao ya kijamii na blogu huku mjadala ukisambaa katika mitaa ya Nigeria.

Mashabiki wa waimbaji wote wawili hatahivyo wamekuwa wakiwatetea wasanii wao huku mjadala ukiendelea.Kituo maarufu cha muziki cha Hip Tv kwa sasa kinafanya kura ya maoni katika X kuhusu nani kati ya wasanii hao ameshinda vita hivyo.

Waimbaji wote wawili wanachukuliwa kuwa nyota wawili wakubwa wa muziki barani Afrika. Wote wameshinda tuzo kadhaa za muziki za MTV na BET na wameshirikiana na wasanii wa kimataifa akiwemo Drake, Chris Brown na Nicki Minaj.

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents