Habari

Deni la Serikali laongezeka lafikia Trilioni 79.1

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema kuwa hadi kufikia Aprili 2023, deni la Serikali limefikia Sh.Trilioni 79.1 sawa na ongezeko la asilimia 13.9 ikilinganishwa na Sh. Trilioni 69.4 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022.

Waziri Nchemba ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha taarifa ya hali ya uchumi atika mwaka 2022 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2023/ 20224 ambapo amesema kati ya fedha hiyo, deni la nje ni Sh. Trilioni 51.2 na deni la ndani ni Sh. Trilioni 2.9.

Amesema ongezeko la duni hilo limetokana na kupokelewa kwa fedha za mikopo kwa ajili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara. Reli, viwanja vya ndege, umeme, elimu na afya.

Aidha amesema tathimni ya uhimilivu wa deni la Serikali iliyofanyika Desemba 2022 imeonesha kuwa ni himilivu na viashiria vya deni viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.

Written by @janethjv255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents