Burudani

Did You know AY yupo chini ya uongozi wa Network Show Biz ya Marekani?

Mafanikio ya Ambwene Yesaya kwenye muziki hayakuja kwa yeye kukaa tu nyumbani na kula starehe. Yametokana na jitihada zake, kutokata tamaa, kijituma, kumuomba Mungu na kuwa karibu na ‘the right people’ kwenye game.
Connection anazozipata za kufanya collabo na wasanii wakubwa wa Marekani kama Romeo (mtoto wa Master P) na Lamyia Good (dada yake na muigizaji maarufu wa Marekani, Meagan Good) zimetokana na watu wanaozijua ramani za muziki wa duniani.
Kama ulikuwa haufahamu ni kwamba AY pamoja na wasanii wengine wanne wakubwa, yupo chini ya kampuni iitwayo Network Show Biz ya Marekani.
Kampuni hii inahusika na production ya muziki na masuala ya kumanage wasanii.
Ina miaka mingi katika kusimimamia kazi za wasanii, kuandaa matamasha ya muziki wa live na kurekodi muziki.
Licha ya AY, Network Show Biz inawasimamia wasanii wengine kama Rachel K, Laymia Good, Ms. Triniti na Town Bidness.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents