Burudani

Diva: Maurice Kirya ni mwanaume special and ‘handsome’ (Video)

Diva the Bawse amemuelezea msanii wa Uganda, Maurice Kirya kama mtu special na anayevutia.

Hiyo ndio maana aliamua kunfollow watu wote kwenye Instagram na kumfollow yeye peke yake. Diva amesema Maurice alimpigia simu kumuuliza kwanini hamfollow mtu yeyote na kumweleza kuwa anataka amani ya moyo lakini msanii huyo akamtishia kuwa kama hivyo basi na naye anamunfollow, kitu ambacho mtangazaji huyo hakuwa tayari.

“Nikamwambia mimi huwa simfollow yoyote but for you I will do something special,” Diva ameiambia Round Up ya Bongo5.

“He is just a special person ndio maana nimemfollow.”

Diva amedai kuwa tayari nchi Uganda msanii huyo amekuwa akipigiwa simu na waandishi wa habari kuulizwa kama ana uhusiano naye kitu ambacho amesema wote wawili hawawezi kusema chochote kwa sasa.

Mtangazaji huyo amesema Maurice ni mwanaume mwenye kila kitu ambacho yeye anakihitaji. “He is really hot halafu he is so nice ukiongea naye, huwa naongea naye muda mrefu, he is such a cool guy. He has everything ambacho mimi as a diva I need in a man.”

Diva amedai kuwa Maurice alimweleza kuwa hana girlfriend na yeye mwenyewe yupo single.

Tazama Round Up hapo juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents