Habari

Dkt. Kigwangalla ampongeza Mbunge wa Kibaha Mjini

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla amekabidhi jumla ya vifaa 831 vyenye shilingi milioni 400, kwa kituo cha Afya Kibaha Mjini, vifaa vilivyotolewa na Mbunge wa jimbo hilo, Silvestry Koka.

Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, Dkt. Kigwangalla alipata fursa ya kukagua maeneo ya majengo ya Kituo hicho cha Afya.

Wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Dkt. Kigwangalla alipongeza juhudi za Mh.Koka kwa kujali wananchi wake kwani hadi kuweza kupata vifaa hivyo aliweza kutumia maarifa na ukaribu wake na wananchi wake hivyo kufika kwa vifaa hivyo vitakuwa faraja kubwa kwa Wanakibaha na wananchi wote wa maeneo jirani.

“Nampongeza Mbunge Koka kwa kuwaletea vifaa hivi. Kwani ni vizuri na vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa Kibaha na maeneo yake ya jirani. Nakupongeza sana sana,” alipongeza Dkt. Kigwangalla

Aidha Kigwangalla aliwataka wananchi wa Kibaha mjini waweze kuwa karibu na Mbunge wao na wamwamini kwani anawajali ndio maana anawatumikia kwa kila njia ikiwemo kuwaletea maendeleo kwa ujumla.

Mbunge wa Kibaha Mjini Mh. Silvestry Koka,Kwa upande wake alimshukuru Dkt. Kigwangalla kwa kuweza kufika na kujionea Kituo hicho pamoja na kukabidhi vifaa. Pia alimuomba kuendelea kufika mara kwa mara kujionea mipango ya Afya katika jimbo hilo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents