Burudani

Dogo Janja adai ukimya wake ulimpa woga jinsi ya kurudi

Rapa Dogo Janja amesema aina ya muziki aliyoifanya kwenye wimbo wake mpya ‘My Life’ alikuwa anatafuta njia ya kurudi kwenye muziki baada ya ukimya wa muda mrefu.
Dogo Janja

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Ijumaa hii, Dogo janja alisema kuwa kabla hajatoa wimbo huo alikuwa ana wasi wasi hukusu mapokezi ya wimbo huo.

“Kitu ambacho kilinifanya nichange style, nilikuwa nafikiria jinsi ya kurudi, pia nilikuwa muoga, nikawa narekodi napeleka, narekodi napeleka, kuna jamaa anaitwa Cal kutoka Norway ni producer alikuja bongo, sasa walikuwa wamenitumia beat, nikaenda studio nikajikuta nimepata melody, michano, nikawatumia michano management yangu wakaona hii inabidi tuiboreshe, ndio ngoma ikatoka”, alisema Dogo janja.

Aliongeza, “Nashukuru sijakutana na changamoto kwani hata watu wananiambia huu ndio muziki wako unakufit, ngoma ina video nimeshoot na hanscana, watu watarajie video mpya na Dogo janja mpya”,

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents