Habari
Video: Dola zaidi ya bilioni 1 zakamatwa Airport
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema zaidi ya dola bilioni 1 zimeshikwa zikiingizwa nchini kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam huku haijulikani zinapelekwa wapi.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo akiwa mjini Dodoma leo wakati akizindua tawi la Benki ya CRDB, amesema kuwa Zaidi ya Dola hizo haijulikani zilikuwa zinaenda wapi.
“Ninapozungumza tu sasa hivi nimepata taarifa zaidi ya bilioni moja Dola zimeshikwa Airport, nasema uongo? zilikuwa zinaingizwa Tanzania na hujui zilikuwa zinaenda wapi, ni kwasababu Tanzania kimeshaonekana ni kichaka cha fedha za kigeni,” amesema Rais Magufuli.